Na Jumia Travel Tanzania
Kipindi
 cha sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka huongoza kwa watu kufanya 
manunuzi ya aina mbalimbali. Ni kipindi ambacho si watu hujikita zaidi 
kwenye kufurahia likizo zao bali hata kuwa huru kutumia pesa kwa ajili 
ya chakula, zawadi na huduma kadha wa kadha.
Kama
 wewe ni mfanyabiashara iwe ya kubwa au ndogo,  kipindi hiki cha mwaka 
huambatana na faida lukuki za kujitangaza na kujitafutia masoko zaidi. 
Yafuatayo ni mambo tisa ambayo Jumia Travel inapendekeza kuwa unaweza kuyatumia kama fursa ili kuwavutia wateja zaidi na kujitangaza katika msimu huu.   
Punguzo la bei.
 Kwa kawaida kipindi kama hiki cha msimu wa sikukuu wateja wengi 
hutegemea punguzo la bei kwenye bidhaa na huduma tofauti. Unaweza 
kuitumia fursa hii kwa kutoa punguzo la bei pia. Mbali na kutoa punguzo 
kwenye biashara yako lakini pia unaweza kushirikiana na wafanyabiashara 
wengine. Kwa mfano, kama unauza nguo unaweza kutoa punguzo la bei ambapo
 wateja wakifanya manunuzi ya kiwango fulani watajipatia fursa ya kupata
 chakula kwenye mgahawa fulani. 
Maazimio ya biashara kwa mwaka ujao.
 Kama ni mfanyabiashara ambaye una dira na malengo ya kuifikisha 
biashara yako mahali fulani lazima utakuwa na maazimio. Unaweza 
kukitumia kipindi hiki kwa kuwajulisha wateja wako maboresho 
unayotarajia kuyafanya mwaka ujao ili kuwavutia zaidi.
Chakula.
 Hakuna mtu asiyependa chakula. Zipo njia nyingi za kuwashukuru wateja 
na wadau mbalimbali waliofanikisha kwa namna moja ama nyingine kufikia 
hapo ulipo. Unaweza ukaanda chakula cha pamoja na kupata fursa ya 
kuzungumza na kujadili masuala mbalimbali yanayoweza kusaidia kukua kwa 
biashara yako. 
Kadi za kushukuru.
 Nguvu ya kushukuru kwa kutendewa jambo fulani ni kubwa tofauti na 
unavyofikiri. Kwa kuonyesha kwamba unajali na kutambua mchango wa wateja
 kwenye biashara yako kunaweza kufungua milango mingi zaidi. Unaweza 
kuandaa kadi zenye ujumbe mzuri wa shukrani na kuwatumia wateja wako 
njia ya barua pepe au kuwapatia pale wanapotembelea biashara yako. 
Mauzo kwa wateja maalumu. Kila
 biashara inakuwa na wateja ambao ni waaminifu kwa namna moja ama 
nyingine. Kwa kutambua mchango wao unaweza kuandaa mauzo maalumu kwa 
ajili yao. Unaweza kulifanikisha hili kwa kuandaa kuponi na kuwapatia 
kisha kuwajulisha kwamba wanaweza kutembelea kwenye biashara yako na 
kufanya manunuzi ya kiwango ulichowapatia. 
Saidia jamii inayokuzunguka.
 Miongoni mwa mbinu ya kujenga uhusiano mzuri na jamii inayokuzunguka na
 ili kukubalika ni pamoja na kutoa msaada kwa masuala mbalimbali. Zipo 
nyanja mbalimbali unaweza kulifanikisha hili. Fanya utafiti mdogo kujua 
changamoto zinazoizunguka jamii yako na kisha omba kutoa mchango wako. 
Inaweza kuwa ni usafi wa mazingira, elimu, watoto yatima nakadhalika. 
Andaa shindano dogo kwa wateja.
 Kama mfanyabiashara unaweza ukaandaa shindano dogo kwa wateja 
wanaotembelea dukani kwako na kisha kujishindia zawadi mbalimbali. 
Unaweza ukaweka tangazo nje ya duka lako ambapo unaweza kuwavutia hata 
wapita njia.    
Andaa burudani kidogo. Haijalishi
 biashara yako ipo kwenye hali gani lakini unaweza ukaanda chochote 
kuwaburudisha wateja wako. Zipo namna nyingi za burudani kama vile 
kuandaa michezo kwa ajili ya watoto au hata burudani ya muziki. 
Tumia mitandao ya kijamii kushirikisha matukio yote.
 Kwa dunia tunayoishi sasa kamwe hauwezi kuidharau nguvu ya mitandao ya 
kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Itumie fursa 
inayoitoa mitandao hii kuwashirikisha wateja wako na jamii kwa ujumla 
mambo yanayotukia kwenye biashara yako na utaona mabadiliko.
Zipo
 njia nyingi ambazo unaweza kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara na 
sehemu tofauti ili kuongeza thamani ya biashara yako. Jumia Travel 
inakushauri kujaribu kufanya kitu tofauti katika biashara yako kabla ya 
mwaka kuisha. Ubunifu ni kitu muhimu ili kukua zaidi lakini pia jifunze 
kutoka kwa wafanyabiashara wengine wanatumia njia zipi kufanikiwa.

Comments
Post a Comment