Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mwaka 2017 uishe, msanii Diamond Platnumz ameachia nyimbo mbili kwa mpigo zikienda kwa majina ya "SIKOMI" na "NIACHE" ambazo zote mbili zimetayarishwa kwenye studio yake ya WCB Wasafi.
Katika nyimbo hizi mbili ambazo kwa kiasi kikubwa ameimba kuhusiana na changamoto zilizomkabili siku chache zilizopita hususani mahusiano yake na Zari pamoja na Hamisa Mobeto.
Sikiliza hapa kwa mara ya kwanza uone ni kwa namna gani Diamond ametumia kipaji chake katika kuelezea hisia zake na kuwaburudisha mashabiki wake kwa wakati huohuo:
Comments
Post a Comment