Mtanzania Mbwana Samatta anayechezea ligi kuu ya Ubelgiji katika timu ya KRC Genk jana usiku ilikuwa kibaruani kwenye uwanja wake wa nyumbani kukabiliana na KAA Gent katika kuwania nafasi ya kuingia robo fainali ya michuano ya kombe la Europa League.
Genk walitinga hautua hiyo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na hivyo jumla ya magoli kuwa ni 6-3 ambapo Samatta katika mchezo wa awali alitupia magoli 2. Hivyo hii inamfanya kuwa mtanzania pekee kufikia mafanikio hayo kuwahi kufanywa na mchezaji yeyote aliyewahi kuchezea nje ya Afrika. Pengine hii inaweza kuwa fursa kubwa kwake kukutana na miamba ya soka duniani kama vile Manchester United, Ajax, Celta Vigo, na wengineo ambao tayari wamekwishatinga hatua hiyo.
Manchester United nao jana walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kuikaribisha timu ya FC Rostov inayoshiriki ligi kuu ya nchini Urusi katika mchezo wa raundi ya pili na kufanikiwa kuwafunga goli 1-0, goli lililowekwa kimywani na mchezaji Juan Mata dakika ya 70 baada ya pasi safi kabisa ya kisigino kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic na kufanya jumla ya magoli kuwa 2-1.
Nimekuwekea matokeo yote kamili na timu zilitinga hatua hiyo ya robo fainali ni KRC Genk, Manchester United, Ajax, Celta Vigo, Lyon, Anderlecht, Schalke 04 na Besiktas.
Comments
Post a Comment