GIGY MONEY ASABABISHA ASABABISHA ALIYEKUWA MSHAURI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO KUJIUZULU


Baada ya kusambaa kwa kipande klifupi cha video kikimuonyesha mwanasheria maarufu kwa sasa nchini ambapo pia anawasimamia wasanii Vaness Mdee na Wema Sepetu, Bw. Albert Msando akiwa anamchezea sehemu za siri msanii Gigy Money ndani ya gari, hatimaye Mkuu wa Chama Cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwake kwenye nafasi aliteuliwa kama mshauri Chama hicho.
Barua hiyo inasomeka kama ifuatavyo:

Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka."

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. 

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo 
Dar es salaam, Mei 23, 2017

Kama ulikuwa bado haujaiona video hiyo, basi itazame hapa chini na utafakari kama ingeweza kupelekea Bw. Msando kufikia maamuzi haya.


Comments