FILAMU YA 'LA LA LAND' YAIBUKA NA TUNZO 6 ZA OSCARS


Jana usiku, Februari 26,2017, zilifanyika tuzo za 89 za filamu za Oscars ambapo filamu ya 'La La Land ilishinda tunzo 6 kati ya vipengele 14 iliyokuwa ikivishindania zikiwemo tunzo za muigizaji bora wa kike na muongozaji bora wa filamu.




Lakini tukio lililoiteka sherehe nzima ya tunzo hizo jana usiku lilikuwa ni baada ya filamu ya 'La La Land' kutangazwa kushinda tunzo ya 'best picture' badala ya filamu ya 'Moonlight' na kuzua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hususani twitter. Tukio hilo lilitokea baada ya waliotakiwa kutangaza na kukabidhi tunzo hiyo kupewa karatasi yenye majina tofauti.



Hata hivyo, baada ya waandaaji kugundua tatizo walirekebisha haraka pale pale jukwaani ingawa tayari washiriki wa filamu ya 'La La Land' walikuwa wamekwishapanda jukwaani.



Ifuatayo ni orodha kamili ya washindi waliobuka kwenye tunzo hizo usiku wa jana.


Tazama picha zifuatazo kuangalia matukio mbalimbali ya washindi wa tunzo hizo:







Comments