Jana usiku kulikuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu ya Uingereza ambapo Leicester City waliikaribisha katika uwanja wao wa King Power.
Leicester wakiwa wametoka kumtimua kocha wao aliyewapandisha daraja na kuwapatia ubingwa wa ligi kuu na kujiwekea historia, Claudio Ranieri, walionyesha kufufuka na kuwashushia kipigo cha magoli 3-1, yaliyofungwa na Jamie Vardy (dakika ya 28 & 60) na Danny Drinkwater dakika ya 39, huku la kufutia machozi la Liverpool lilifungwa na Felipe Countinho katika dakika ya 68.
Kufungwa huko kwa Liverpool ambayo ipo nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kunaipa nafasi nzuri Manchester United ambao wao wamekuwa king'ang'anizi kwenye nafasi ya 6 tangu mwezi Oktoba mwaka jana.
Pia katika mchezo huo wa jana, mashabiki wa timu ya Leicester waliitumia fursa ya mchezo huo wa jana kutoa shukrani zao kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo aliyewapatia ubingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza, Claudio Ranieri, aliyefukuzwa baada ya matokeo mabaya ya timu hiyo.
Tazama picha za matukio yalivyokuwa yakiendelea uwanjani hapo kwenye picha zifuatazo:
Comments
Post a Comment