Katika kudhihirisha kwamba vya kale ni dhahabu, msanii Rayvanny ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'SIRI' akiwa amemshirikisha Nikk wa Pili. Kumbuka kwamba msanii maarufu wa bendi nchini, Hussein Jumbe alikwishawahi kuwa na kibao kikiitwa 'Mapenzi ya Siri' ambacho kilitamba na bado kikipigwa hata leo hakiishi utamu.
Kuonyesha kwamba anathamini mchango wa wakongwe hao kwenye muziki nchini Tanzania, Rayvanny amemtumia Jumbe kama sehemu ya watu waliocheza kwenye video hiyo. Itazame hapa kwa mara ya kwanza:
Comments
Post a Comment