ITAZAME HAPA VIDEO YA DIAMOND NA OMARION

Machi 14, Diamond Platnumz alizindua albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la 'A Boy From Tandale' huko jijini Nairobi, Kenya. Kwenye uzinduzi wa albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo 20, 10 ambazo zimeshasikika huku 10 zikiwa mpya kabisa, Diamond alimualika msanii kutokea nchini Marekani ambaye hapo nyuma pia aliwahi kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya nyimbo pamoja naye.

Masaa machache baada ya uzinduzi wa albamu hiyo, Diamond ameachia rasmi video ya wimbo alioshirikiana na msanii huyo unaokwenda kwa jina la 'AFRICAN BEAUTY', ambao kwa mara ya kwanza ulichezwa na video kuonyeswa jukwaani.

Wimbo umetayarishwa na Laizer wa studio za Wasafi wakati video ikiongozwa na Justin Campos kutokea Afrika ya Kusini, itazame hapa kwa mara ya kwanza:


Comments