DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU ALBAMU, MAHUSIANO, KUFUNGIWA NYIMBO ZAKE, KUBANIWA NA 'MEDIA' ZINGINE

Sidhani kama kuna mtu hafahamu kwamba siku chache zilizopita kwamba Diamond Platnumz alizindua albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la 'A BOY FROM TANDALE' jijini Nairobi, Kenya. Sidhani kama kuna mtu pia hafahamu kwamba wakati yupo kwenye harakati hizo nyimbo zake mbili za 'WAKA' na 'HALLELUJAH' zilikutana na rungu la kufungiwa na BASATA pamoja na Wizara yenye dhamana. 

Sidhani kama kuna mtu pia hafahamu vuguvugu alilonalo Chibu kwenye mahusiano yake ya kimapenzi baada ya kuachana na mpenzi wake Zari pamoja na kususiwa kuchezwa kwa nyimbo zake pamoja na za wanamuziki wake wa kundi la WCB na baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Mashabiki wa muziki wa msanii huyu pamoja na watanzania kwa ujumla walikuwa wanasubiria kwa hamu kuhusu maelezo yake binafsi kuhusiana na masuala yote hayo. Na kwa sasa ni miongoni mwa masuala yanayogonga vichwa vya habari mbalimbali ndani na nje ya nchi pamoja na kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Baada ya kufanya mahojiano na vyombo vya habari mbalimbali nchini Kenya kuhusuiana na masuala hayo, kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kutoka kwenye uzinduzi wa albamu yake nchini humo, mtangazaji Lil Ommy ambaye anatangaza kipindi cha 'The Play List' kinachorushwa na kituo cha Times FM alibahatika kufanya naye mahojiano ya kwanza kabisa. 

Katika mahojiano hayo Diamond licha ya kujibu maswali mbalimbali ya kichambuzi kuhusiana na albamu yake, pia alifafanua baadhi ya mambo ambayo mashabiki wake walikuwa na kiu ya kuyasikia. 

Kama ulipitwa au haukubahatika kuyaona mahojiano hayo, nimekuwekea hapa video kwa hisani ya LilOmmy TV, karibu uitazame.


Comments