VIDEO MPYA: Unique Sisters - Kwako Wewe

Baada ya kimya kirefu cha zaidi ya miaka 10, miongoni mwa waasisi na makundi ya mwanzo kabisa ya wadada kwenye 'gemu' la muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania, Unique Sisters wamerudi tena.

Kundi la wadada hao ambao lilikuwa linaundwa na ndugu watatu liliwahi kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo ile ya 'Baishoo' ya mkongwe mwingine ambaye yupo kimya naye, Mack D.

Hii hapa ni video ya wimbo wao mpya baada ya kuuliziwa sana na mashabiki walioufanya kwenye studio za Fishcrab chini ya mtayarishaji Lamar:


Comments