Agosti 13 ni siku muhimu sana kwa muziki wa hip-hop nchini Tanzania kwani ni kumbukizi ya kuzaliwa kwa msanii mahiri kabisa kuwahi kutokea, Fareed Kubanda al-maarufu kama Fid Q, Tajiri wa Mashairi na Flow au Ngosha kama mwenyewe anavyopenda kuitwa na mashabiki wake.
Katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kwake, Fid Q huwa ana utaratibu wa kuachia kazi mpya ikiwa ni kama zawadi kwa watanzania wote wanaopenda kuziki wake. Na katika siku hii Ngosha aliachia kazi mbili ambazo ni 'Ulimi Mbili' ikiwa ni audio peke yake akiwa amewashirikisha Maua Sama, Hard Mad na Noorelly; na 'Fresh' ambayo ametoa video maridadi kabisa ikiwa imefanywa na mtayarishaji Tiddy Hotter na kuongozwa na Destro. Zisikilize na kuzitazama hizo kazi hapa chini:
Comments
Post a Comment