Hakuna anayeweza kubisha kwamba kutumika kwa vionjo vya nyimbo ya Salome iliyoimbwa na mwanamuziki Saida Karoli miaka kadhaa iliyopita kwenye nyimbo za Salome ya Diamond akiwa na Rayvanny, Muziki ya Darassa na Give To Me ya Belle 9 ndicho kilichomrudisha mwanamama huyo kwa kasi kwenye anga ya muziki nchini na mashabiki kutamani kumsikia tena.
Bila ya ajizi Saida Karoli ameitikia wito huo kwa kuja na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la "Orugambo" chini ya mtayarishaji Tud Thomas, ambamo ndani yake pia ametumia vionjo vya maneno ya nyimbo za wasanii hao wa bongo flava. Itazame video ya wimbo huo mpya kwa mara ya kwanza hapa ikiwa imeongozwa na Hanscana:
Comments
Post a Comment