Baada ya minong'ono ya chini kwa chini kuhusu mahusiano ya kimapenzi baina ya wasanii wawili wanaofanya vizuri kwenye anga ya muziki wa bongo flava Vanessa Mdee na Jux kuwa yamefikia tamati hatimaye ukweli umejulikana.
Kupitia mahujiano na kituo cha redio cha Soundcity cha nchini Nigeria, Vanessa Mdee aliulizwa kuhusu jamaa aliyeonekana kwenye video ya wimbo wa ''Juu' ambao aliufanya pamoja na Jux kama ni kweli ni wapenzi maana walisikia kuwa ni wapenzi. Na je kuachana kwao kumesababishwa kwa namna moja ama nyingine kutokana na masuala ya polisi 'kutajwa kwake kwenye ishu ya kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.'
Vanessa Mdee alijibu kuwa, "Tulikuwa pamoja lakini kwa sasa hatuko tena. Kulikuwa na mengi yaliyokuwa yakiendelea kipindi hiko, na ninafuraha kwamba wote wawili tulikivuka kikwazo kile. Anaendelea vizuri kwa sasa na ana nyimbo mpya" na mimi ninafurahi kufikia hapa nilipo, basi ni hivyo tu."
Nimekuwekea hapa video ya mahojiano hayo yalivyokuwa, tazama:
Comments
Post a Comment