VIDEO MPYA: Reekado Banks ft Vanessa Mdee - Move

Hii inaweza kuwa ni 'kolabo' ya nne kama sikosei kwa msanii Vanessa Mdee kufanya na wasanii kutokea nchini Nigeria, ya kwanza ilikuwa na Ice Prince Zamani, ya pili na Orezi halafu akafanya ngoma ya 'Dwasi' kupitia 'beat' aliyopewa na mtayarishaji mahiri, Legendary Beatz.

Safari hii ameshirikishwa tena kwenye nyimbo mpya iliyomo kwenye albamu ya 'Spotlight' ya msanii Reekado Banks kutokea lebo kubwa ya muziki nchini Nigeria inayomilikiwa na Don Jazz, unaokwenda kwa jina la "Move."

Hii ni dalili nzuri kwa muziki wa Tanzania kwani ukiachana na akina AY, ALI KIBA, DIAMOND, na JOH MAKINI, kwa mwaka huu kusema ukweli Vanessa Mdee ameipeperusha vema bendera ya taifa letu kimataifa na tunatarajia kolabo za kutosha mpaka mwaka huu unaisha.

Itazame video hapa kwa mara ya kwanza nimekuwekea;


   

Comments