Baada ya Harmonize na Rich Mavoco kuachia kichupa chao kipya cha wimbo wa 'Show Me' ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye chati mbalimbali za muziki nchini Tanzania, msanii mwingine kutoka lebo ya WCB ameachia video mpya.
Si mwingine bali ni Rayvanny V Vanny Boy ambaye siku za hivi karibuni ameonekana akiwa jijini Nairobi nchini Kenya kwenye kipindi cha Coke Studio, naye ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Zezeta" ambao 'audio' yake aliiachia siku chache zilizopita.
Wakati ngoma ikiwa imetayarishwa na Lizer wa studio za WCB, Rayvanny amesafiri mpaka jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini na kumpatia kazi muongozaji Nic Roux, itazame hapa kwa mara ya kwanza:
Comments
Post a Comment