Akizungumzia
juu ya huduma hiyo mpya kwenye mtandao wa kampuni hiyo, Meneja Mkaazi
kwa hapa Tanzaia, Bi. Fatema Dharsee amesema kwamba dhumuni kubwa ni
kuonyesha kuwajali na kuwazawadia wateja wao waaminifu wanaotumia huduma
zao mara kwa mara kwa ajili ya malazi au kukata tiketi za ndege.
“Lengo
kubwa la Jumia Travel ni kuhakikisha kuwa tunawezesha huduma za malazi
na usafiri ndani na nje ya Afrika kuwa rahisi na nafuu. Kwani tunaamini
kwamba licha ya gharama ambazo mteja atazitumia lakini bado anastahili
ubora wa hali ya juu na uzoefu wa kipekee. Kwa kufanya hivyo itamfanya
aendelee kutumia huduma zetu zaidi na hata kuwashawishi watu wake wa
karibu kufanya hivyo pia,” alisema Bi. Dharsee.
“Kupitia programu hii mpya tuliyoizindua, inamaanisha kwamba sasa wateja ambao wamekuwa wakitumia mtandao wetu kupata huduma za malazi na usafiri wa ndege mara kwa mara watapatiwa ofa za punguzo la bei ambalo wateja wengine hawawezi kuzipata wala kuziona. Wateja wengine wa kawaida watakaokuwa wanatembelea mtandao wetu wataona bei za kawaida na sio za ‘travel smart’ Ili kunufuaika na huduma hii mpya lazima mteja awe amejisajili au kuwa na akaunti kwenye mtandao wa travel.jumia.com ndipo ataweza kuziona ofa hizo kutoka kwa hoteli mbalimbali tulizoingia nazo makubaliano,” alihitimisha Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini.
Programu hii mpya ya ‘travel smart’ kutoka kwa Jumia Travel
pia itakuwa na manufaa makubwa kwa hoteli washirika kwani itawawezesha
kuona idadi ya wateja waliosajiliwa na huduma hii kwani wao pekee ndio
wanaweza kuzifaidi ofa hizi. Hii itazisaidia hoteli zao kuonekana au
kutangazwa zaidi na kuwaongezea masoko kupitia kampeni maalum
inayofanyika kuitangaza miongoni mwa wateja.
Comments
Post a Comment