Msanii wa Bongofleva, Dogo Mfaume amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akithibitisha kifo cha msanii huyo ambaye moja ya kazi zake ni wimbo unaojulikana kwa jina la 'KAZI YA DUKANI' mmiliki wa 'Sober House' alikokua akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema kuwa afya Dogo Mfaume ilikua nzuri kabisa na alikua ana mwaka mmoja toka ameacha utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ na tulikua tumejiandaa kesho twende tukamtolee damu.
Amesema alikua afanyiwe upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na tayari ameshapangwa kwenye ratiba.
"Afya yake ilikua nzuri kabisa na aliniambia dada mimi sitaki kuondoka kwako nataka unisimamie kila kitu na sitaki kurudi mtaani, mtaani hali mbaya na nikikaa kule nitarudi kutumia unga” amesema mmiliki huyo wa Sobber House.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mali pema peponi
Comments
Post a Comment