DIDDY ACHOMOZA KINARA TANO BORA YA WASANII WA HIP-HOP WANAOINGIZA MKWANJA MREFU ZAIDI DUNIANI




Kwa mara nyingine tena msanii P. Diddy amewaongoza wasanii wa hip-hop nchini Marekani kwa kuibuka kinara kwa upande wa kutengeneza mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka 2017.

ORODHA YA WASANII WA HIP-HOP WANAINGIZA PESA NYINGI DUNIANI - KWA MUJIBU WA FORBES:

  1. Diddy - Dola za Kimarekani milioni 820
  2. Jay Z - Dola za Kimarekani milioni 810
  3. Dr. Dre - Dola za Kimarekani milioni 740
  4. Birdman - Dola za Kimarekani milioni 110
  5. Drake - Dola za Kimarekani milioni 90


Msanii huyo ambaye ndiye mmiliki wa lebo kubwa ya muziki duniani iliyowatoa wasanii akiwemo marehemu Biggie Smalls au 'B.I.G' amevuta jumla ya dola za Kimarekani milioni 820 na hivyo kumfanya aongoze orodha hiyo. Utajiri wa Diddy umetokana na mauzo makubwa kupitia Ciroc Vodka, Revolt TV, ziara yake aliyoifanya ya muziki iliyokwenda kwa jina la 'Bad Boy Family Reunion Tour' na vitega uchumi vingine.

JAY Z, gwiji mwingine wa muziki huo ndiye anayemfukuzia kwa karibu sana huku yeye akiwa na utajiri wa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 810. Utajiri wake kwa kiasi kikubwa unatokana na umiliki katika mtandano wa muziki wa TIDAL, Roc Nation, na kupitia biashara mbalimbali ambazo ana ubia nazo, ikiwemo dili lake la kutengeza filamu za luninga na kampuni ya The Weinstein.


Katika orodha hiyo nafasi ya tatu inashikiliwa na mtayarishaji nguli wa muziki wa hip-hop duniani, Dr, Dre ambaye wasanii wengi mashuhuri wamepitia kwake akiwemo marehemu Tupac na sasa Kendrick Lamar ambaye anatamba kwenye chati mbalimbali za muziki duniani ikiwemo Billboard. Dre yeye ameiingiza jumla ya dola za Kimarekani milioni 740 ambapo pesa hizo zimechangiwa kwa kiasi kikubwa na mkataba mnono wa mabilioni ya dola ambayo haujawahi kuingiwa hapo kabla kwa mwaka, dola za Kimarekani bilioni 3 kupitia 'headphones' zake za Beats by Dre aliouingia na kampuni ya Apple.


wanaofuatia kwenye orodha hiyo, nambari nne ni mmiliki wa lebo ya muziki ya Cash Money, Birdman, akiwa na utajiri wa dola za Kimarekani milioni 110 ambapo anawamiliki wasanii kama vile Lil Wayne, Drake na Nicki Minaj. 


Na nafasi ya tano yupo msanii Drake ambaye yeye ana jumla ya mkwanja wa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 90 ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mauzo ya albamu yake VIEWS, lebo yake ya mavazi ya OVO, ziara ya muziki ya 'Summer Sixteen Tour,' Virginia Black pamoja na mikataba minono ya kibiashara ya kampuni za Apple na Nike.


Orodha hiyo ya mwaka huu haina tofauti sana na ya mwaka jana kwani pia iliongozwa na Diddy na kufuatiwa na Dr. Dre, Jay Z, Birdman na Drake.   

    

Comments