WEUSI WAELEZEA KWANINI WALIKATAA KUPIGA SHOO UCHAGUZI MKUU 2015

Kundi la wanamuziki wa miondoko wa Hip-Hop linalojulikana kwa jina la WEUSI ambalo maskani yake kuu ni mkoani Arusha limeweka wazi kwanini walivichomolea vyama kadhaa vya siasa licha ya kupokea simu zao za kuwataka kwenda kutumbuiza kwenye majukwaa yao ya kampeni.

Akizungumza mmoja wa wasanii wanaowakilisha kundi hilo, Niki wa Pili wakati wa mahojiano ya kipindi cha luninga cha FNL kinachorushwa na luninga ya EATV kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 3 usiku alisema kuwa walikataa kwa sababu, "SISI TUNAJIHUSISHA NA SIASA ZA WANANCHI NA SIO SIASA ZA WANASIASA."

Niki aliendelea mbele kwa kufafanua kuwa, "Kama tungekubali kufanya shoo kwenye jukwaa lolote lile la chama cha siasa wakati wa uchaguzi maana yake tungekubali kuingia na kutumiwa kwenye siasa za wanasiasa wakati hilo sio lengo letu sisi. Sisi kupitia muziki tunaofanya ni kwa ajili ya wananchi, watanzania wote yaani kwa maneno mengine tunazungumzia masuala yanayowahusu wao na si wanasiasa."

Kundi hilo ambalo kwa sasa linafanya vizuri na wimbo wao mpya wa "Madaraka ya Kulevya" ambao bado ni tata kwa wengi wa mashabiki kutokana na mafumbo mengi yaliyozungumzwa ndani yake. Usikilize vizuri hapa chini:




Comments