Meneja na mtangazaji wa redio wa muda mrefu nchini Tanzania ambaye anaongoza kuwatoa wanamuziki wengi wa bongo flava, Sandu George a.k.a KID BWAY kupitia lebo yake ya muziki ya TETEMESHA ENTERTAINEMENT, amekuja na msanii mpya anayekwenda kwa jina la COYO.
Kama ulikuwa haujui Kid Bway ndiye aliyewatoa akina Barakah The Prince (Siachani Naye), Sajna (Iveta), C Sir Madini na wengineo wengi tu kutokea jijini Mwanza.
Safari hii amekuja na msanii mwingine mpya ambaye anafanya muziki wa Hip-Hop, msanii huyu ana uwezo mkubwa wa kuimba na kurap, lakini kikubwa anafananishwa na DARASA kutokana na staili anayofanya pamoja na hata muonekano wake:
Itazame hapa video ya wimbo huo iliyoongozwa na muongozaji NISHER ambaye anaonekana kama amerudi tena kwa kasi ya ajabu:
Comments
Post a Comment