Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imepewa pointi tatu na magoli matatu baada ya kikao cha kamati ya Saa 72 kuthibitisha kuwa mchezaji Fakhi Mohammed wa Kagera Sugar alikuwa na kadi tatu za njano katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Aprili 2,2017 katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
“Mchezaji huyu alipata kadi ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Mbeya City, akapata kadi nyingine ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Maji Maji na pia alipata kadi ya njano kati ya mchezo wa Kagera Sugar na timu ya African Lyons,” alisema Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Yahaya.
Faki alicheza kwenye mchezo wa Kagera Sugar na Simba uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba ambapo timu yake ilimzamisha Mnyama kwa mabao 2-1.
Sasa Simba wapo kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara wakiwa na Pointi 61 huku Yanga wakishika nafasi ya pili wakiwana Pointi 56.
Comments
Post a Comment