Gwiji la muziki wa Hip-Hop nchini Marekani na mfanyabiashara mkubwa kwa sasa akiwa anamiliki vitega uchumi kadhaa pamoja na vinginevyo lukuki vikiwa njiani, JAY Z ameongeza mkataba wa lebo yake ya muziki ya Roc Nation kuendelea kufanya kazi na Live Nation.
Huku mkataba wao wa sasa wa miaka 10 wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 360 ukielekea ukingoni mwaka ujao, pande hizo mbili zimesaini tena mkataba mwingine wa muda mrefu ambapo makubaliano hayakuwekwa wazi, kwa mujibu wa Billboard.
"Live Nation ina makubaliano ya ushirikiano wa muda mrefu na Jay Z, na tunatarajia kuendelea kuwa washirika wenye usawa wa kibiashara kwenye Roc Nation kwa miaka mingi ijayo," alisema msemaji.
Kwa mujibu wa taarifa, hii haiwezi kuwa kuongezwa kwa muda kwa mkataba wa zamani bali ni mpya kabisa katika baishara za Jay Z. Jigga pamoja na Live Nation wanatarajiwa kuendelea kuiendesha Roc Nation kwa pamoja.
Hapo mwanzo, kulikuwa na tetesi kwamba huenda Jay Z angeipeleka Roc Nation kushirikiana na Universal Music Group. Kwa mujibu wa taarifa, tetesi hizo hazikupatikana.
Taarifa hizi za 'dili' jipya la Hov linakuja huku kukiwa kuna taarifa zikisambaa za yeye kuja na albamu yake peke yake pamoja na ya yeye kushirikiana na mkewe, Beyonce. Imepita miaka minne sasa tangu aachie albamu ya Magna Carta....Holy Grail, lakini hivi karibuni, alishirikiana na wasanii Frank Ocean na Tyler, the Creator kwenye ngoma ya ''Biking'' pamoja na Beyonce kwenye nyimbo ya DJ Khaled ya ''Shining.''
Jay Z kazi zake kama mfanyabiashara zinazidi kushamiri, ambapo hivi karibuni anatarajia kuzindua kampuni ya 'venture capital,' pamoja na ofa za filamu na luninga kutoka kwa kampuni ya Weinstein.
Comments
Post a Comment