CHEKI VIDEO MPYA YA FRENCH MONTANA ALIYOIFANYIA NCHINI UGANDA

Unakumbuka kwamba msanii wa muziki wa Hip-Hop kutokea nchini Marekani kutokea lebo ya Bad Boy Entertainment inayomilikiwa na P. Didy, French Montana alikuwa anashea picha kwa mashabiki wake kwamba yupo nchini Uganda anafanya 'documentary'???

Yap! Basi dokumentari hiyo imezaa video ya wimbo wake mpya wa "UNFORGETTABLE" aliyomshirikisha msanii mmojawapo wa kundi la RAE SREMURRD anayejulikana kwa jina la SWAE LEE.

French Montana ambaye ni mzaliwa wa nchini Morocco barani Afrika, ameamua kuachia wimbo huu baada ya kuandamwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kutoa maneno machafu kwa mwanamke wa kiafrika.

Lakini Montana aliomba msamaha kwamba hakukusudia hayo kwani yeye mwenyewe ni muafrika na amezaliwa na mama wa kiafrika ukiachilia mbali ameoa mwanamke muafrika. Hivyo amejaribu kuelezea hiyo ndo dunia tunayoishi sasa hivi ambapo mtu ukijaribu kuzungumza akili yako lakini mitandao ya kijamii hubadili mambo na kuvumisha vitu tofauti.

Itazame video hiyo hapa chini:



Comments