Mchana wa leo UEFA walichezesha droo kwa ajili ya nusu fainali za vikombe vya UEFA CHAMPIONS na EUROPA LEAGUE.
Katika kombe UEFA CHAMPIONS LEAGUE zilikuwa zimebaki timu nne ambazo ni Real Madrid na Atletico Madrid zote za nchini Hispania; Juventus ya Italia na AS Monaco ya Ufaransa.
Droo iliyochezeshwa leo imezikutanisha tena timu hasimu kutokea jiji la Madrid ambazo ni Real na Atletico Madrid, hivyo mashabiki watajionea tena MADRID DERBY nyingine kwenye UEFA ambapo katika matokeo ya mahasimu wao walifungana goli 1-1 mnamo Aprili 8, 2017.
Mchezo wao wa nusu fainali utachezwa siku ya Jumanne ya Mei 2, 2017 ambapo Real Madrid watakuwa nyumbani kuwakaribisha Atletico Madrid na kurudiwa juma linalofuata. na kama mambo yakiwaendea vizuri Real Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane inaweza kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa kombe hilo.
Natika nusu fainali ya pili ambayo itazikutanisha timu za Monaco ya Ufaransa na Juventus ya Italia itachezwa siku ya Jumatano ya Mei 3, 2017 na kurudiwa juma linalofuata. Juventus watasafiri mpaka Ufaransa kuvaana na timu hiyo yenye chipukizi wengi machachari kama vile Kylian Mmbape na nahodha wao Ramadel Falcao ambaye kama vile amefufuka baada ya kutofanya vizuri wakati akiwa ligi kuu ya Uingereza.
Timu mbili kati ya hizo nne zitakazoshindana zitacheza fainali ya kugombea kikombe siku ya JUMAPILI ya JUNI 3, 2017 jijini Cardiff nchini Wales.
Droo nyingine ilikuwa ni ya nusu ya kombe la EUROPA LEAGUE ambapo timu nne ziliingie ambazo ni Manchester United ya Uingereza, Celta Vigo ya Hispania, Lyon ya Ufaransa na Ajax ya Uholanzi.
Katika michuano hiyo ambayo wengi wanaiangalia timu ya Manchester United inayonolewa na kocha Jose Mourinho ikipambana kurudi kwenye michuano ya UEFA aidha kupitia kushinda kombe hili au kupenya nafasi nne za juu za ligi ya Uingereza ambapo kuna changamoto kubwa kweli.
Manchester United katika droo hiyo amepangwa na Celta Vigo huku Lyon ya Ufaransa ikipangiwa na Ajax, timu kutokea Uholanzi ikiwa ni baada ya miaka saba bila ya hali hiyo kutokea.
Raundi ya kwanza ya michezo hiyo itachezwa siku ya Alhamisi ya Mei 4, 2017 na kurudiwa juma linalofuata tarehe 11.
Timu mbili kati ya hizo nne zitakazoshindana zitacheza fainali ya kugombea kikombe siku ya JUMATANO ya MEI 24, 2017 jijini Stockholm nchini Sweden.
Comments
Post a Comment