ALBAMU YA KENDRICK LAMAR KINARA KWA SASA CHATI ZA BILLBOARD 200


Wiki moja tu tangu aachie albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la "DAMN," imetosha kumfanya mwanahip-hop huyo kutokea Compton, Kendrick Lamar kuongoza kwenye chati za albamu bora ya Billboard 200.

Albamu hiyo iliyofanywa na lebo za TDE/Aftermath/Interscope imefanikiwa rasmi kufikia rekodi kubwa ya mwaka kwa mara ya kwanza baada ya uzinduzi ambapo imeibuka kinara kwenye chati za mauzo kwa njia ya mtandao au 'Sales Plus Streaming (SPS)' kwa kufikia 610,000 ndani ya wiki moja tu.

Kendrick ameipiku albamu ya Drake, More Life iliyotayarishwa na YMCMB/Republic ambayo kwa mauzo ya 505,000 ndiyo ilikuwa ikishikilia rekodi kubwa ya SPS mpaka hivi sasa. 

Hata hivyo Lamar pia ameivunja rekodi ya msanii kutokea nchini Uingereza, Ed Sheeran ya kuwa na mauzo makubwa ndani ya wiki moja tu ya mwaka; ya albamu ya Divide iliyofanywa na Atlantic, ambapo ilifungua wiki kwa mauzo 350,000 ya albamu huku DAMN mpaka hivi sasa imekwishafikia takribani 362,000.     

Comments