WIZKID KUMSHIRIKISHA DRAKE KWENYE "COME CLOSER"


Baada ya nyimbo ya "One Dance" ya Drake aliyomshirikisha kufanya vizuri mpaka kufikia nambari 1 kwenye chati za billboards na nyinginezo duniani na pia kutangazwa na mtandao wa kununua na kusikiliza nyimbo kwa njia ya mtandao wa Spotify kuwa ndio wimbo uliovunja rekodi kwa kusikilizwa zaidi duniani, wasanii hao kushirikiana tena.

Safari hii Wizkid ambaye anafanya vizuri barani Afrika na duniani kwa ujumla kupitia miondoko ya muziki wa afropop anatarajia kumshirikisha mmarekani huyo kwenye wimbo wake mpya kutoka katika albamu yake ya tatu (Sounds From Other Side) utakaokwenda kwa jina la "Come Closer," chini ya lebo ya muziki ya RCA Records.


Wizkid aliwafahamisha mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo alisema, "Ilinichukua miaka 3 kuamua kuingia makubaliano na lebo hii. Lengo lilikuwa sio pesa bali ni muziki. 'Come Closer,' wimbo wa kwanza. Mungu anatuongoza.. 31-3!"



Comments