Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame M. Mbarawa, leo amezindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila ya kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana kitaalamu kama (Mobile Number Portability(MNP).
Zifuatazo ni baadhi ya picha wakati wa uzinduzi huo:
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame M. Mbarawa akiongea na wadau mbalimbali wa Masuala ya Mawasiliano wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya kuhama mtandao mmoja kwenda mwingine bila ya kubadili namba ya simu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame M. Mbarawa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Vodacom Tanzania, Nina Pendael Eshun (kulia) pamoja na wadau wa masuala ya mawasiliano baada ya uzinduzi wa huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila ya kubadili namba ya simu (Mobile Number Portability)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame M. Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wanaotoa huduma za mawasiliano za simu za mkononi mara baada ya kuzindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana kitaalamu zaidi kama (Mobile Number Portability (MNP).
Wageni na wadau waalikwa wa sekta ya mawasiliano wakifuatilia kwa ukaribu uzinduzi rasmi wa huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila ya kubadili namba ya simu. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania, (TCRA) leo jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment