WAFANYAKAZI 9 WASIMAMISHWA TBC


Wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), wamesimamishwa kazi kwa kosa la kurusha habari ya uongo iliyotolewa na mtandao wa Fox Channel ambao ni maarufu kwa ‘kutunga’ na kusambaza habari batili.
Rungu hilo limewashukia wafanyakazi hao kutokana na kurusha habari ya uongo iliyochapishwa na mtandao huo iliyodai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu Rais John Magufuli na kwamba ametoa nafasi ya upendeleo kwa Watanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amethibitisha kusimamishwa kwa wafanayakazi wa shirika hilo.
“Ni kweli, watu kadhaa wamesimamishwa kutokana na suala hilo,” Dkt. Rioba anakaririwa na Mwananchi.
Majina ya wafanyakazi waliosimamishwa ni pamoja na Gabriel Zacharia ambaye alionekana akiisoma habari hiyo wiki iliyopita, wengine ni Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Juica Losai.
Mtandao wa Fox ni moja kati ya mitandao mikubwa nchini Marekani ambaye imekuwa ikitunga na kuandika habari batili zinazoibua mikanganyiko na mara kadhaa huviingiza kwenye mtego vyombo vingi vya habari hususan tovuti.

Comments