VIDEO YA WIMBO WA SOUNDTRACK YA 'THE FATE OF THE FURIOUS '


Kama sio mpenzi wa mfululizo wa filamu za 'Fast and Furious' basi inabidi uzitafute na uziangalie kwani ifikapo April 14 mwaka huu itatoka filamu ya 8 katika mfululizo huo inayokwenda kwa jina la 'The Fate of the Furious' ambapo tuliona katika iliyopita ilikumbwa na msiba mzito baada ya muigazi mmojawapo, Paul Walker kupoteza maisha kwa ajali mbaya ya gari.

Hapa nimekuwekea video mpya ya wimbo uliofanywa kwa ushirikiano wa wasanii G-Eazy na Kehlani unaokwenda kwa jina la 'Good Life.' 

Ndani ya video ya wimbo huu utaona vipande tofauti tofauti vya filamu hiyo ambayo imechezwa na waigizaji maarufu kama vile Vin Diesel, Dwayne 'The Rock' Johnson, Tyrese na Ludacris.

Itazame hapa chini nimekuwekea: 


Comments