Imeonekana YOUNGKILLA MSODOKI hakufurahishwa kabisa na "maneno maneno" yaliyoibuka baada ya kuachia ngoma yake ya SINAGA SWAGGER ambayo haina muda mrefu tangu itoke.
Miongoni mwa mstari ulioibua hisia na ukakasi kwa mashabiki wengi wa muziki pamoja wanamuziki wenzake na wadau mbalimbali wa muziki ni juu ya kugusia kuwa "kwa jinsi mtaani wanavyosema JOH MAKINI anabebwa inamfanya na yeye aanze kuamini kuwa ni kweli."
Basi kuanzia hapo ikawa ndio mada ya mazungumzo kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, mashabiki, wanamuziki, wadau wa muziki na hata kundi la WEUSI wenyewe kuhoji ukomavu wa msanii huyo mpaka kufikia hatua ya "KUMDISS" JOH MAKINI.
Youngkilla hakupendezwa na jinsi watu walivyopokea mstari huo kwa ujumla na alivyotafsiriwa kwani alidai hakumaanisha hivyo bali ni sehemu ya yeye tu kujiuliza. Wimbo wake ulipatwa kuongelewa sana na kuitwa vya kutosha kwenye mahojiano na vituo mbalimbali vya habari.
Sasa basi kuona hiyo haitoshi kwa kuelezea nia yake, YOUNGKILLA MSODOKI ameamua kama kujibu flani hivi kupitia remix ya SINAGA SWAGGER REMIX, icheki video hapa chini nimekuwekea ikiwa imeongozwa na mtayarishaji NICKLASS:
Comments
Post a Comment