VIDEO MPYA: Professor Jay - Kibabe

Gwiji wa muziki wa Hip-Hop nchini Tanzania, The Heavy Weight MC, Jay wa Mitulinga, Mti Mkavu, Professor Jay hayo yote ni majina yake lakini siku hizi ameongeza jina jipya tena lenye hadhi mbele ya jamii, Mh. Mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya CHADEMA ameachia video mpya inayokwenda kwa jina la 'Kibabe.'

Professor Jay ni miongoni mwa wasanii wakongwe nchini ambao bado wanawasumbua wasanii wa sasa kwa kutoa kazi mpya na zinazofanya vizuri.

Katika nyimbo hii mpya Jay amezungumzia vitu vingi sana ambavyo vimetokea hapa kipindi cha katikati hasa baada ya kutoa ngoma yenye mahadhi ya singeli aliyomshirikisha Sholo Mwamba.

Humu kazungumzia suala hilo, umoja, ugomvi katika sanaa, harakati za kisiasa, mafanikio binafsi na muziki, na mengineyo mengi.

Kwa mujibu wake video hii imefanyika sehemu tofauti pamoja na Mikumi mkoani Morogoro ambalo ndio jimbo lake, amefanya hivyo pia kama kuwapa fursa watu kujionea jimbo lake na fursa za kitalii zinazopatikana kule.

Karibu uitazame hiyo video hapa chini iliyofanywa na muongozaji Hanscana:


Comments