Jay Moe kaamua kwenda sawa na wasanii wa kizazi cha sasa kwa kwenda nao mulemule, ila kwa spidi hii 'Mzee Famous' naona kama anawachachafya vijana. Baada ya kuja vizuri na kutamba na Pesa Ya Madafu sasa kadondosha mzigo mwingine uniatwa 'Nisaidie Kushare.'
Bonge la 'idea' la nyimbo ambayo hakuna mtu aliyewahi kufikiria, na hii ni ndio maana ya ubunifu katika sanaa. Bila ya kusahau video nzuri iliyofanywa na Kwetu Studio chini ya muongozaji Msafiri 'Travellah,' ni level za mbele kabisa zimefanyika humu ndani.
Idea ya wimbo ni mpya kabisa katika tasnia ya bongo flava, na ujumbe unaendana na mazingira yaliyopo ambayo ni kasumba ya wasanii wetu kupiga 'promo' za kufa mtu halafu kinakuja kutoka kitu kinyume na matarajio ya wengi.
Karibu uitazame hapa chini na usaidie 'KUSHARE' kama More Techniques anavyosisitiza:
Comments
Post a Comment