Naweza kusema Barakah The Prince ni bingwa wa nyimbo za kulalamika kutoka kiwanda cha bongo flava nchini Tanzania, tangu nyimbo ya kwanza anatoa mahadhi ni yaleyale na hivyo kujitengenezea mashabiki wake wa kutosha.
Msanii huyo kutoka lebo ya muziki ya ROCKSTAR4000 ametoa nyimbo mpya inayokwenda kwa jina la 'Acha Niende' aliyoifanya studio za AM records chini ya BOB MANECKY na MANECKY mwenyewe huku video ikifanywa na Kevin Bosco Jnr wa kutoka nchini Kenya.
Cha kuvutia kwenye video hii ni msanii nguli nchini Kenya na Afrika ya Mashariki, PREZZO kutumika ndani yake, nadhani nawe utapigwa na butwaa kwa kudhani labda ameshirikishwa kuimba, la hasha!
Tazama video nimekuwekea hapa chini;
Comments
Post a Comment