Msanii wa kike wa bongo flava nchini, Vanessa Mdee au 'Cash Madame' kama anavyopenda kuitwa na mashabiki wake kwa sasa amejisalimisha Makao Makuu ya Polisi baada ya kutakuwa kufanya hivyo alipotajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.
Msanii huyo ambaye alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya shughuli za muziki na utengenezaji wa tamthiliya ya 'SHUGA' alikuwa ni mmojawapo wa wasanii na watu kadhaa mashuhuri nchini waliotajwa na Mkuu wa Mkoa kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Mwanasheria wake, Aman Tenga amethibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha kituo kikuu cha Polisi mara baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Mkuu wa Mkoa.
Wakili Tenga alifafanua zaidi kuwa mteja wake ambaye alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya majukumu ya kikazi wakati jina linatajwa, Amethibitisha pia kuwa polisi walifika nyumbani kwake Kunduchi na kupekua kabla ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya vipimo kabla ya kuwekwa ndani.
Comments
Post a Comment