Baada ya kuchukua likizo ya ghafla na ya muda mfupi baada ya sekeseke la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia studio za Clouds Media Group wiki chache zilizopita, watangazaji Soudy Brown na Kwisa Thompson au SHILAWADU kama wanavyojulikana na wengi kupitia kipindi chao kinaruka kwenye luninga ya Clouds TV wametangaza kurejea tena.
Wakizungumza kwenye video fupi hapa chini wamesema kuwa iliwabidi kuchukua likizo hiyo fupi kwa ghafla na wanawaomba radhi mashabiki wao ili Ijumaa ya leo watakuwepo tena hewana kama kawa tena wakiwa na "UBUYU" wa kutosha tu. Itazame video hapa chini (Video kwa hisani ya GLOBAL TV).
Comments
Post a Comment