TAZAMA MATUKIO MBALIMBALI NAMNA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ILIVYOSHEREHEKEWA TANZANIA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amelaani na kukemea vikali vitendo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinavyoendelea katika jamii na amewataka wananchi kote nchini kushirikiana katika kukabiliana na vitendo hivyo nchini. 


Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya. 


 Akina mama wajasiliamali wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baad ya kushiriki mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na Vodacom Tanzania leo  katika maadhimisho ya siku ya wananawake Duniani.


Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazee wa Kituo cha Mother Theresia Kigogo leo baada ya kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


Baadhi ya wanawake wakijumuika pamoja na Shirika la Equality for Growth (EfG), katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na shirika hilo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.



Comments