Mbali na kuwa muimbaji mzuri wa muziki, Rihanna pia anajishughulisha na shughuli za kusaidia jamii ambapo mwaka 2014 aliweza kuzindua taasisi aliyoiita jina la Clara Lionel Foundation (CLF) ikiwa ni kama kumbukumbu ya babu na bibi zake.
Baada ya kutangazwa na Chuo Kikuu cha Havard cha nchini Marekani mwaka jana kuwa mshindi wa tunzo bora ya mwaka kwa kujihusisha na kusaidia jamii, Rihanna anaendelea na juhudi zake za kusaidia jamii ambapo kwa mara ya kwanza ataadhimisha miaka 3 ya taasisi hiyo jijini New York.
Tukio hilo linalokwenda kwa jina la "Diamond Ball" litafanyika Septemba 14 katika ukumbi wa Capriani Wall Street, ambapo ndipo sehemu yenyewe ambayo msanii huyo alikuwa akiihitaji. Katika maadhimisho hayo anatarajia kusherehekea mafanikio ya kazi nzuri ya taasisi hiyo pamoja na kukuza hamasa ya malengo yake duniani.
Kwa kawaida taasisi ya CLF hujishughulisha na harakati za kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta za elimu na afya duniani kote.
Kwa mara ya kwanza alizindua tamasha la "Diamond Ball" mwaka 2014 ikihudhuriwa na Brad Pitt, Kim Kardashian na Big Sean. Mwaka uliofuatia wa 2015 alifanya pia msimu wa pili na kuhudhuriwa na Will Smith, Kylie Jenner, Zendaya na Kevin Hart.
Comments
Post a Comment