Ikiwa hata wiki moja haijakwisha tangu aachie albamu yake ya 9 "Rather You Than Me", msanii Rick Ross atangaza ujio wa albamu yake ya 10.
Hayo alizangumza wakati wa mahojiano na kituo cha Miami cha The Beat 103.5 ambapo aliulizwa ni nini kinafuatia baada ya kuachia albamu yake ya 9, Ninataka kukamilisha miaka 10 kwa kutoa kitu cha 10, albamu yangu ya 10, kabla sijaufunga mwaka wangu wa 10, itakwenda kwa jina la Port of Miami 2: Born To Kill," alisema Rozay.
Msanii huyo ambaye pia ni bosi wa lebo ya muziki ya Maybach Music Group aliachia albamu yake kwa mara ya kwanza mwaka 2006 ambapo ndani yake kulikuwemo ngoma kali iliyomtambulisha kwenye ulimwengu wa muziki, "Hustlin" pamoja na "Push It."
Tazama mahojiano hayo kwenye video hapa chini:
Comments
Post a Comment