Bosi wa lebo ya muziki ya Maybach Music Group (MMG), RICK ROSS, ambayo ndani yako wapo wasanii MEEK MILL kutokea Philadelphia na WALE kutokea Wshington DC, jana ameweka wazi kuwa alimuonya MEEK kuhusu uhusiano wake na Nicki Minaj.
Ross, amezungumza wakati alipoalikwa kwenye kipindi cha Wendy Show kinachoendeshwa na mwanadada Wendy Williams kuwa, alimuonya Meek kama mdogo wake kuwa makini na mahusiano hayo, na kamwe asingeweza kumzuia kuingia kwenye mahusiano hayo kwani kama mdogo wake alitambua kuwa naye alikuwa na nafasi ya kufurahia maisha.
Kwenye kipindi hiko azungumzia pia kuhusu maisha yake binafsi, ujio wa albamu mpya pamoja na kumchana bosi wa lebo ya muziki ya CASH MONEY juu ya kuwanyonya DJ KHALED na LIL WAYNE.
Tazama kwenye video hapa chini kwenye mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji Wendy kwenye kipindi chake:
Comments
Post a Comment