Msanii Nay wa Mitego amekamatwa na polisi mkoani Morogoro na kupelekwa kituo kikuu cha Mvomero leo asubuhi akiwa hotelini alikofikia mara baada ya kumaliza shughuli zake zilizompeleka kule.
Nay ambaye ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la "Wapo," aliwafahamisha mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kuandika maneno, "Nimekamatwa kweli. Muda huu nikiwa hotel Morogoro mara baada ya kumaliza kazi yangu iliyonileta. Napelekwa Mvomero Police. Nawapenda watanzania wote #Truth#Wapo."
Sababu kubwa kwa kukamatwa kwa msanii huyo inawezekana ikawa ni wimbo wake mpya wa "WAPO" ambao ndani yake amezungumzia masuala mengi tofauti hususani yanayotokea nchini Tanzania kwa wakati wa sasa ambapo yameigusa serikali kwa namna moja ama nyingine.
Comments
Post a Comment