MKE WA T.I. KUMBE ALISHIRIKI KWENYE UANDISHI WA 'SHAPE OF YOU' YA ED SHEERAN


Je ulikuwa unajua kwamba mke wa mwanamuziki maarufu wa Hip-Hip kutokea Atlanta, Georgia nchini Marekani, T.I., bi shosti Tameka "Tiny" Cottle ameshiriki kwenye uandishi wa nyimbo inayoshikilia nambari moja kwenye chati ya nyimbo bora 100 za Billboard, Shape of You ya muingereza Ed Sheeran?

Hayo yamejulikana leo baada ya Ed Sheeran kuweka furaha yake wazi kushilia nafasi hiyo kwa wiki 7 mfululizo kwa kushea habari hiyo nzuri kupitia ukurasa wake wa twitter.

Tiny hakuwa peke yake kwenye uandishi wa nyimbo hiyo bali pia walishirikiana na Kandi Burruss na mwandishi mwingine anayejulikana kwa jina la Kevin "Shek'spere" Briggs.


Kwa Tiny hii ni nyimbo yake ya pili kufikia mafanikio hayo baada ya pia kushiriki kwenye uandishi wa nyimbo za kundi la TLC ya "No Scrubs" wakati kwa Kandi kwake yeye ni ya tatu kwani licha ya kushiriki kwenye hizo nyimbo mbili pia alishiriki pia kwenye uandishi wa nyimbo ya kundi la Destiny's Child ya "Bills, Bills, Bills." 


Kandi na Tiny kwa pamoja waliwahi kuwa kwenye kundi moja la muziki la Xscape ambapo hivi karibuni limerudi pamoja kufanya kazi. 

Kwa wengi wanamfahamu Tiny kwa sababu ya kuwa mke wa msanii T.I na pia kumuona kwenye ushiriki wa kipindi chao cha TV cha "The Family Hustle," lakini Kandi Burruss yeye ni mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo, lakini pia ni msanii wa kwenye vipindi vya TV ambapo anashiriki kwenye mfululizo wa vipindi vya "The Real Housewives of Atlanta."

Tazama video ya Ed Sheeran ambaye imetoka takribani mwezi mmoja hapa chini:



Comments