MAN UTD YATOLEWA FA CUP


Jana usiku katika uwanja wa 'Stamford Bridge' jiji la London lilizizima kwa mtanange wa kufa mtu ulizikutanisha timu za Chelsea na Manchester United katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho la Uingereza au 'FA Cup.'




Katika mchezo huo ambapo Manchester United walicheza pungufu wakiwa wachezaji 10 baada ya Ander Herrera kupewa kadi ya pili ya njano na hivyo kutolewa nje, N'Golo Kante ndiye alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga goli la pekee dakika 6 baada ya kipindi cha pili (51).



Comments