MAN CITY NJE MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA


 

Manchester City jana usiku iliweka rekodi ya kipekee baada ya kuwa timu iliyoshinda magoli 5 katika raundi ya kwanza ya hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya na kutolewa kwenye raundi ya pili.


Timu hiyo inayoshirika ligi kuu ya Uingereza na kuongozwa na kocha Pep Guardiola imetolewa kwa geni la ugenini na Monaco ya Ufaransa baada ya kufungwa magoli 3-1 licha ya mchezo wa kwanza kushinda magoli 5-3.


Magoli ya Monaco jana yalifungwa na kinda Klyian Mbappe Lottin dakika ya 8, akiwa amefunga jumla ya magoli 11 kwenye michezo 11 aliyoichezea timu hiyo msimu huu, huku la pili na la tatu likifungwa na wachezaji Fabinho dakika ya 29 na Tiemoue Bakayoko dakika ya 77, wakati goli la Manchester City likifungwa dakika ya 71 na Leroy Sane.



Kwa kocha Pep Guardiola ambaye amekwishanyanyua kombe hilo mara 2 wakati akiifundisha timu ya Barcelona, ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya kufundisha soka kuondolewa kwenye hatua hiyo.


Hivyo basi baada ya Manchester City kuondolewa jana inamaanisha kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Leicester City ndiyo timu pekee inayoiwakilisha nchi hiyo katika hatua ya robo fainali baada ya kutinga juzi usiku kwa kuichapa Sevilla ya Hispania magoli 2-0.


Katika mchezo mwingine uliopigwa pia jana usiku Atletico Madrid walipita hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Bayer Leverkusen baada ya mchezo wa kwanza kuwafunga 4-2. 

Comments