Malkia wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Lady Jaydee anatarajia kuzindua albamu yake ya 7 tangu aanze kufanya shughuli za muziki. Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyika siku ya Ijumaa ya leo pale katika ukumbi wa King Solomon Hall uliopo Kinondoni kuanzia saa 3 usiku.
Jide kama anavyojulikana kwa wengi amekuwa ni hamasa kubwa kwa wanamuziki wengi wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa na ameiwakilisha Tanzania vizuri kimuziki barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Comments
Post a Comment