KIWANDA CHAFUMANIWA KIKIWA NA VIROBA WAKATI AGIZO LA KATAZO LIKIWA LIMEANZA




Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA ), Emmanuel Alphonce akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya operesheni ya viroba katika kiwanda cha nyati sprit leo Vingunguti jijini Dar es Salaam.



Vijana wakipanga Viroba katika boksi walipokutwa na timu ya operesheni viroba iliyofika katika kiwanda cha Nyati Spirit leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


Sehemu ya Katoni za Viroba vilivyokutwa katika kiwanda cha nyati sprit leo jijini Dar es Salaam.


Mafisa wa serikali wakikagua nyaraka mbalimbali za kiwanda cha Nyati Sprit ikiwa ni uhalali wake wa kuendelea kufanya biashara katika mfumo mpya kutoendelea.


Utekelezaji wa operesheni hiyo umeanza kufanyika leo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipotangaza marufuku hiyo Februari 20 juu ya vileo vilivyo katika vifungashio viondoke katika mzunguko wa biashara na watengenezaji wahamie katika mfumo wa chupa kwa kuanzia milimita 250.

Operesheni ya kukamata viroba imeanza leo jijini Dar es Salaam ikisimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Katika Kiwanda cha Kampun ya nyati spirit kilichopo Vingunguti ambapo katoni za viroba 7067 aina ya nyati  zimekutwa katika kiwanda hicho.

Akizungumza katika operesheni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA ), Emmanuel Alphonce amesema operesheni imeanzia jiji la Dar es Salaam na kesho itaendelea nchi nzima chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rupa Suchik amesema hatatengeneza tena viroba ikiwa ni agizo la serikali na vilivyopo watateketeza . Amesema kuanzia jana ameshapunguza wafanyakazi 150 kutoka 300 kutokana na agizo hilo na hao wataingia katika mfumo wa uzalishaji vileo katika mfumo wa Chupa.

(Habari kwa msaada wa: Chalila Kibuda, Globu ya Jamii)

Comments