Juventus anaongoza ligi hiyo akiwa na alama 67 nyuma ya AS Roma wenye alama 59 wakati AC Milan wao wakiwa nafasi ya 7 na alama 50 tu.
Pia mchezo huu unaweza kuwa ni fursa nzuri kwa mshambuliaji wa Juventus, Gonzalo Higuain kushika usukani kwa kuongoza katika ufungaji wa magoli ambapo kwa sasa anafungana na Edin Dzeko wote wakiwa na magoli 19, huku wakifuatiwa kwa ukaribu kabisa na mshambuliaji wa FC Napoli, Dries Mertens, mwenye magoli 18 na Mauro Icardi wa Inter Milan akiwa na 17.
Ligi hii ya Serie A kwa sasa nchini Tanzania unaweza kuiona kupitia king'amuzi cha StarTimes pekee, kwani wao ndio wenye hakimiliki ya kurusha matangazo ya michezo yote ya ligi hiyo moja kwa moja.
Comments
Post a Comment