JUMIA TRAVEL YAJITANUA KWENYE MIJI MIPYA AFRIKA NA DUNIANI

Jumia Travel inazidi kuimarisha uwepo wake duniani katika sekta za hoteli, usafiri na mazingira ya utalii kwa kutambulisha maeneo mapya ndani na nje ya bara la Afrika.     

Kampuni hiyo imefikia idadi ya hoteli zaidi ya 30,000 kwenye orodha yake barani Afrika na zaidi ya 300,000 duniani kote, miaka minne tu tangu kuanza shughuli zake mnamo mwaka 2013. Hii inajumuisha maeneo mapya katika miji mashuhuri Afrika kama vile Afrika ya Kusi
ni, Morocco, Misri na Tunisia, pamoja na nje ya mipaka ya Afrika ambayo ni Dubai, London, New York, Paris na Maka (Mecca) miongoni mwa mingineyo.

Katika kuhakikisha kuendelea kutoa huduma ubora, bosi wa Jumia Travel, Paul Midy amesema, “Tunao uwezo wa kutosha kabisa kuwafanya washirika wetu kujulikana  kimataifa, na kutoa suluhu kwa wateja wetu, katika mahitaji yao yote ya usafiri mahali popote duniani.”

Hatua hii imelenga kuwawezesha waafrika wengi zaidi kupanua mipaka yao ya kusafiri ndani na nje. Sehemu ya mpango huu ni kuwawezesha wateja kuwa na vifurshi vya kusafiri kwenda maeneo mapya, huduma kwa wateja masaa 24 siku zote za wiki, ushauri wa kitaalamu pamoja na njia rahisi za malipo kupitia machaguo tofauti kama vile Tigo Pesa, kulipa unapowasili, na kadi ya malipo (credit card).


Vifurushi hivyo vitajumuisha muda wa kukaa hotelini, tiketi za ndege za kurudi, upatikanaji wa huduma ya matembezi kama itahitajika. Ila havitajumuisha gharama za kupata pasi ya kusafiria, bima ya kusafiria, pamoja na huduma nyinginezo ambazo hazikuorodheshwa hapo juu.

“Wasafiri wengi wanabadili mwelekeo wao kutoka kwenye bidhaa za pamoja badala yake wanataka zile zinazowalenga na kuwapatia machaguo binafsi zaidi. Kwa hiyo tunafanya kazi na hoteli zetu kwa ukaribu zaidi pamoja na washirika wengine wa usafiri mitandaoni kuwapatia wateja huduma zinazokidhi mahitaji na machaguo yao duniani kote,” aliongezea Midy.

Kifurushi cha kwanza kimeulenga mji wa Dubai kama mahali ambapo wateja wengi watautembelea kwenye mapumziko ya sikukuu zijazo za Pasaka.
Hivi karibuni Jumia Travel ilizindua huduma za ndege, ikiwa ni jitihada za kuufanya mtandao wake barani Afrika kumuwezesha msafiri kujipatia huduma zote anazozihitaji sehemu moja.

Naye kwa upande wake Meneja Mkaazi wa kampuni hiyo nchini Tanzania, Fatema Dharsee amebainisha kuwa, “Ni hatua kubwa kwetu sisi na wateja kwa ujumla kuwawezesha kusafiri kwenda miji mingi mashuhuri zaidi duniani. Huduma hii imekuja muda muafaka ambapo hivi karibuni pia tulizindua huduma za ndege. Lengo letu kubwa ni kuwawezesha wateja ambao watahitaji kwenda sehemu zingine duniani kufanya hivyo kupitia mtandao wetu tofauti na awali ambapo ilibidi kwenda mitandao mingine.”



Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja inayoongoza kwa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika. Humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya 30,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 300,000 duniani kote.
Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Kabla ya mwezi Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas.

Comments