Ifahamu miji ya kitalii inayotembelewa zaidi Zanzibar


Na Jumia Travel Tanzania

Je unaifahamu vipi Zanzibar kwa upande wa sehemu za kitalii ambazo watalii wengi hupenda kutembelea? Unadhani utaweza kumsaidia mtu akikuuliza kuhusu visiwa hivyo na akapata ufahamu wa kutosha?

Wengi wanaifahamu Zanzibar kama sehemu ya nchi ya Tanzania inayojumuisha visiwa vya Unguja na Pemba. Kuijua kwa undani zaidi Jumia Travel imeangazia sehemu tofauti ambazo ni lazima uzijue kama ukitembelea huko.    
Huu ndio mji mashuhuri na wa kipekee zaidi katika visiwa vya Zanzibar (Unguja) kutokana na kuwa na historia ndefu. Ukiwa hapa utavutiwa na mandhari nzuri ya majengo mbalimbali ya miaka ya nyuma yaliyojengwa karne ya 19 yenye mchanganyiko wa mataifa kama vile Waarabu, Wahindi, Waafrika na Wazungu. Na hii ndiyo sababu kubwa iliyopelekea mnamo mwaka 2000 shirika la umoja wa kimataifa linalojishughulisha na masuala ya elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) liliutangaza Mji Mkongwe wa Zanzibar kuwa ni sehemu ya urithi wa dunia.

Sehemu wanazopenda kuzitembelea watalii katika mji huu ni kama vile; Mji Mkongwe, Makumbusho ya Kasri ya Sultan, Nyumba ya Maajabu, Nyumba ya Livingstone, Zahanati ya Kale, Kanisa la Kianglikana na eneo la Forodhani.

Nungwi inapatikana kaskazini mwa Zanzibar ambapo ni hupendelewa zaidi na watalii kwa shughuli za kuogelea. Eneo hili liko umbali wa takribani saa moja mpaka mawili ukiwa unatokea Mji Mkongwe. Safari za kwenye boti huku ukitazama jua likizama pia ni shughuli maarufu zinazopendwa na watalii wakitembelea eneo hili.

Takribani kilometa 3 Kusini mwa Nungwi unapatikana mji wa Kendwa ukiwa na fukwe safi na za kuvutia. Zipo shughuli nyingi za kufanya kama vile kushiriki kuvua samaki na wavuvi au kwenda kupiga mbizi chini ya bahari. Pia eneo hili kunakuwa shughuli mbalimbali za kiburudani zinazoandaliwa kama vile tukio maarufu la “Fool Moon Party” ambalo huandaliwa na Kendwa Rocks na kuvutia umati mkubwa na wasanii mbalimbali.   



Hiki ni kijiji kidogo cha kijadi kilichopo Kaskazini Mashariki mwa pwani ya Zanzibar. Kikiwa kinapakana na sehemu kubwa ya fukwe ya bahari pia kuna hoteli na nyumba za kulala wageni. Lakini pia sehemu hii ipo karibu na kisiwa maarufu cha Mnemba. Unaweza kufika Matemwe kwa njia tofauti kama vile; kutokea Mji Mkongwe kwa njia ya teksi au kwa daladala lakini pia kwa njia teksi ukitokea Nungwi.   

Ni kijiji kilichochangamka kinachopatikana Kusini Mashariki mwa Zanzibar kikiwa ni maarufu kwa michezo ya baharini, kupiga mbizi, fukwe na migahawa ya kuvutia. Unaweza kujifunza mila na tamaduni mbalimbali kijijini hapa lakini pia kujifunza michezo ya kuteleza kwenye bahari pamoja na kuogelea.  

Ni kijiji kidogo cha kivuvi Kusini Mashariki mwa pwani ya Zanzibar, takribani kilometa 10 Kusini mwa mji wa Paje. Kijiji hiki kina hoteli na nyumba za kulala wageni za kutosha hivyo suala la sehemu ya kufikia sio tatizo. Kusini mwa eneo hili pia kunapakana na vijiji vya Bwejuu na Paje. Usafiri wa kufika Jambiani kutokea Mji Mkongwe ni rahisi na hausumbui au unaweza kuwasiliana na hoteli unayokwenda kufikia ili kukusaidia kwa hilo. Furahia safari za kwenye mitumbwi ili kujionea kuzama kwa jua ukiwa baharini pamoja na miamba ya kuvutia ya matumbawe.

Kusini Mashariki mwa Zanzibar kunapatikana Michamvi, eneo ambalo limeingia baharini kidogo na kujulikana kijiograjia kama Peninsula. Ukitembelea hapa utaweza kufurahia fukwe safi za bahari huku kukiwa na hoteli na nyumba za kulala wageni kwa gharama nafuu zaidi. Eneo hili ni tulivu ukilinganisha na Kaskazini, hivyo kutoa fursa nzuri kwa wanaokwenda kwa ajili matembezi na famili au kupumzika kwa wanandoa.

Eneo hili linapatikana Kusini Mashariki mwa Zanzibar unapatikana mji wa Makunduchi. Eneo hili ni maarufu kutokana na tukio kubwa la “Mwaka Kogwa” ambalo hufanyika kati ya mwezi Julai na Agosti. Hii huwa ni sherehe ya kusherehekea tamaduni na mwaka mpya wa washirazi visiwani Zanzibar. Kihistoria washirazi ndio walikuwa wageni wa kwanza kutoka nje ya Afrika kufika visiwani humo na hivyo utamaduni wao umeenea na kufuatwa na watu wengi.



Ni kijiji cha wavuvi kinachopatikana Kusini Magharibi mwa Zanzibar. Siku za hivi karibuni eneo hilo limekuwa maarufu miongoni mwa watalii hata kwa safari za boti baharini pamoja na kuogelea pamoja na pomboo “Dolphin.”

Tunaamini kwamba kwa makala haya utakuwa umepata angalau ufahamu wa namna gani Zanzibar ilivyo. Kitu cha kustaajabisha kuhusu visiwa hivi na kwamba karibuni kila sehemu ni kivutio kwa watalii.

Comments