Ratiba ya nusu fainali ya kombe la FA CUP ilikuwa inasubiria kumalizika mchezo wa jana kati ya Chelsea na Manchester United ili kuungana na timu ambazo zilikwishapita katika hatua hiyo Tottenham, Arsenal na Manchester City. Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kushinda goli 1-0, lililowekwa kimyani na N'Golo Kante dakika ya 51.
Baada ya mchezo huo ratiba ya nusu fainali ilitoka baada ya masaa machache baadaye ambapo Chelsea watakutana na Tottenham siku ya Aprili 22 huku Arsenal yeye akipangiwa Manchester City siku ya Aprili 23.
Ratiba kamili nimekuwekea hapa chini:
Comments
Post a Comment