Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mara baada ya mahubiri katika Kanisa hilo. Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Waumini wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.
Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200 ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo.
Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha ambazo ni utekelezaji wa Ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya ziara mkoani humo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa.
PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment